![]() |
SUNDAY MANARA |
Miaka kadhaa nyuma Baba yangu na shujaa wangu Mohammed Ramadhan Manara(Sunday Manara)Maarufu kama Computer alizaliwa, ninaishuhudia siku hii adhimu kwa my dady na kwangu nikiwa mwenye furaha tele,huku mvua inayonyesha leo ikiongeza furaha hii.
Ndiye Mtanzania pekee uliyecheza na Pele katika kikosi cha New York Cosmo, pia ulicheza na Jomo Sono.
Hakika
wewe ni shujaa halisi wa taifa hili, ukiwa Mtanzania wa kwanza kuwa
profesional footboler tena ktk level kubwa unapaswa kuenziwa ukiwa hai.
![]() |
SUNDAY MANARA (WA PILI KULIA) WAKATI AKIKIPIGA ULAYA. |
Najua
ukitangulia mbele ya haki mengi kukuhusu yatasemwa,hasa historia yako
murua ya kandanda lakini mimi mwanao nakuenzi leo na siku zote,naambiwa
ww ni best player of all time ktk taifa hili.
Hakika
ni kujivunia kunakostahiki kwangu, kitu kikubwa ni kuachia maamuzi
yangu ktk mambo makhsuus, kama kuamua kupenda klabu yangu maalum ya
Simba SC ilhali wewe ni legend wa Yanga.
Sizisahau
zama zile nikilazimisha uninunulie jezi nyekundu na hukusita,
naikumbuka pia ile siku niliyotia viatu vyako kwenye pipa la maji,ili tu
usichezae ktk game ya Pan African na Simba, but siku zote uliacha
mahaba yangu kwa Simba yawe huru. Kila ulichonipa baba nakikumbuka
sana,kuanzia shule,madrasa na hata ushauri wako pia....nakupenda mzee
wangu na jivunie mimi,
HAPPY BIRTHDAY
Ni mimi mwanao Haji S.Manara
Post a Comment