Kila
siku panapokucha kila mmoja huianza mihangaiko ya siku akitarajia kuwa
kile anachokifanya kitamwezesha kufanikiwa na siku moja ataishi maisha
ambayo anayatamani.Watu wengi wakiwa katika
mihangaiko hiyo kuna mtu ambaye tayari amefanikiwa (role models) huwa
wanamuangalia wakitamani kufanikiwa kama yeye au hata zaidi yake. Wakati
mwingine watu hawa hutumia muda wao na wale wanaowaiga ili waweze
kuwaambia ni njia gani walizoweza kuzitumia wakafanikiwa na kufika hapo
walipo.Lakini watu husema huwezi ukamuuzia
adui ramani ya vita. Japo hapa si suala la uadui lakini usitegee
akwambie kila kitu. Ukweli ni kuwa kuna mambo ambayo hatokwambia ili
aweze kujihakikishia kuwa anapunguza ushindani. Hapa chini ni orodha ya
mbinu 13 za kufanikiwa kifedha ambazo rafiki yako tajiri hatakwambia.1.
Anatumia kidogo kuliko anachopata. Anaweka akiba zaidi. Anafahamu ni
bora kuwa tajiri usiyejulikana kuliko kuwa masikini na kuishi kwa
kujifanya tajiri.2. Anajua kwamba uvumilivu
unalipa. Lakini uvumilivu bila juhudi hauna maana. Ukifanya kazi leo
ukitarajia kesho uwe bilionea utakuwa hauishi katika uhalisia. Mafanikio
ni zao la muda.3. Ukienda kwake utakuta chai,
mlo kamili na vitu muhimu mezani. Huwezi kukuta kanunua kitu ambacho
hakina faida kwa mwili zaidi ya matatizo.4.
Hapendi madeni na akiwa nayo anayalipa. Hanunui kitu kwa mkopo bila
sababu ya msingi. Anafahamu kwamba Kama kitu huwezi kukulipia cash basi
huna uwezo nacho na ni budi ukajipanga upya.5.
Anafahamu kwamba uhuru wa kifedha ni jambo la nafsi. Uhuru wa kifedha
maana yake kuishi bila deni na sio kuwa na fedha lukuki na madeni lukuki
wakati huo huo.6. Anafahamu kwamba kuwa na
shughuli mbili za kufanya sio tu kwamba kunakuongezea kipato lakini pia
kunakunyima muda wa kutumia fedha vibaya kwa kukuweka ‘bize’.7. Anafahamu Pesa ni kama mtoto mdogo, haiwezi kujisimamia na kujiongoza yenyewe, lazima uisimamie wewe mwenyewe.8. Anafahamu kwamba utajiri wa kweli mara nyingi unakuja unapofanya kitu unachokipenda.9. Anajua ukishindwa kuwa na mipango maana yake unajikosesha mafanikio tayari.10. Haishi kwa kuwaza kushindwa. Anafahamu mwanzo wa mafanikio ni kujiamini.11. Anajua kwamba muda sio rafiki wa binadamu. Kwa hiyo anaheshimu muda kwa kiwango cha juu kabisa.12.
Anafahamu kwamba huwezi kutumia usicho nacho. Hawazi kuanza kutumia
fedha kabla hajaifanyia kazi. Haishi katika ndoto anaishi katika
uhalisia.13. Anakushangaa kwamba unaendesha
gari ya milioni 14, mkeo gari ya milioni 12, na wote ofisini zenu ziko
karibu karibu, na magari yote ya mkopo na umepanga nyumba vya vyumba 5
wakati una mke na watoto wawili tu.USIONDOKE KWENYE POST HII BILA KU SHARE NA MARAFIKI ZAKO JAPO WA 5 TU ILI UKOMBOE MAISHA YAO.
Asante sana kwa technology na full computer couse visit medtechnicstz.com
ReplyDelete