Siku chache kufikia siku ya utoaji tuzo za Soundcity MVP, Kituo cha TV cha Sound City kimetangaza list ya kwanza ya wastaa wa muziki watakaoperform kwenye sherehe hizo na zipo taarifa kuwa kutakua na suprise performance ya mastaa kutoka Tanzania wametajwa kuperform siku hiyo.soundcitymvp-15538526_758122051004656_7225151954228346880_n 
List ya kwanza ya wasanii watakaopanda kwenye steji ya SoundCityMVP2016 ni pamoja na Davido, Patoranking, Tekno, na Olamide huku mshereheshaji wa siku usiku huo atakuwa ni Bright Okpocha a.k.a Basketmouth, comedian kutoka Nigeria.
Kwa mujibu wa waandaji wa tuzo hizo wameeleza kuwa list ya wasanii watakaoperform siku hiyo itakuwa na mastaa kutoka Tanzania, South Africa na Nigeria ambao wataonekana live kutoka kwenye ukumbi wa Expo Center, Eko Hotel & Suites jijini Lagos, Nigeria.
Inaelezwa kwamba zaidi ya watazamaji milioni 50 kutoka Afrika watashuhudia utoaji wa tuzo hizo kwa njia ya TV pamoja na wale watakaokuwa live ukumbini. Tuzo hizi zinatarajiwa kutolewa tarehe 29 December, na unaweza kuwapigia kura wasanii kutoka Tanzania kwa kuingia hapa soundcitymvp.com.
Mwisho wa kupiga kura ni December 27, 2016.


PICHA:Tazama party ya Belle 9 iliyofanyika nyumbani kwa Ridhiwani Kikwete


Ni mwimbaji mwingine staa wa bongofleva ambaye bado yuko kwenye game na juzi ameachia video yake mpya ft. G Nako ‘give it to me‘ na party ya Waalikwa maalum ilifanyika nyumbani kwa Ridhiwani Kikwete Dar es salaam, tazama kwenye hii video hapa chini

Post a Comment

 
Top