Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
MAKAMU
wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani
Jumanne Nyamlani leo amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania Urais wa
shirikisho hilo katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu Dodoma.
Nyamlani
alikuwa Makamu wa Rais wa TFF, chini ya Rais Leodegar Chilla Tenga kati
ya Desemba 14, mwaka 2008 na Oktoba 27, mwaka 2013.
Akawa mpinzani mkuu wa rais wa sasa wa TFF, Jamal Emil Malinzi katika uchaguzi uliopita Oktoba 27, mwaka 2013, lakini akashindwa baada ya kupata kura kura 52 dhidi ya 72 za ‘mbabe wake’.
Nyamlani
anafanya idadi ya watu sita hadi sasa waliojitokeza kuchukua fomu za
Urais, pamoja na Malinzi wengine ni Katibu wa zamani wa TFF, Frederick
Mwakalebela, Mwenyekiti wa zamani wa Yanga, Wakili Imani Madega, Makamu
wa Rais wa sasa wa TFF, Wallace Karia na Fredrick Masolwa.
Athumani Nyamlani amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania Urais wa TFF katika uchaguzi wa Agosti 12, mwaka huu Dodoma
Katika
nafasi ya Umakamu wa Rais ni waliochukua fomu hadi sasa ni Mulamu
Nghambi, Michael Wambura na Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ambao wanachama wa
klabu ya Simba. Kaburu ni Makamu wa Rais wa Simba kwa sasa.
Nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni waliochukua fomu leo hadi sasa saa 6.30 mchana ni Lameck Nyambaya, Omar Ali, Abdallah
Mussa, Peter Steven, Said Tulliy, Ally Mussa, Mussa Kisoki, Salum
Chama, Ephraim Majige, Elias Mwanjala, Saleh Alawi, Kaliro Samson,
Vedastus Lufano, Kenneth Pesambili, Mbasha Matutu, Samuel Daniel,
Dunstan Mkundi, Athumani Kambi, Shaffi Dauda, Golden Sanga, Charles
Mwakambaya, Benista Rugola, Thabit Kandoro na Goodluck Moshi.
Wengine
ni James Mhagama, Hussein Mwamba, Sarah Chao, Issa Bukuku, Stewart
Masima, Emmanuel Ashery, Abdul Sauko, Mussa Sima, Stanslaus Nyongo,
Ayoub Nyenzi, John Kadutu, Baraka Mazengo, Khalid Mohamed, Mohamed Aden,
Cyprian Kuyava na Saleh Abdul.
Uchaguzi
Mkuu wa TFF umepangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma
wakati zoezi la kuchukua fomu litakamilika Juni 20, mwaka huu na kikao
cha mchujo wa awali kwa wagombea kitafanyika Juni 21 mkapa Juni 23.
Juni
24 na 25, mwaka huu, kamati itafanya kazi ya kuchapisha na kubandika
kwenye mbao za matangazo majina ya wagombea wakati Juni 26-28 zitakuwa
siku za kupokea na kuweka mapingamizi kwa wagombea na Juni 29 mpaka
Julai Mosi itakuwa kipindi cha kupitia mapingamizi yote na kufanya
usaili.
Kwa
mujibu wa Kuuli, Julai 2-3 kitakuwa kipindi cha kuchapisha na kubandika
matokeo ya usaili, Julai 4-7 na kipindi cha Sektretarieti kuwasilisha
masuala ya Kimaadili kwenye Kamati ya maadili, Julai 7-11 ni kipindi cha
kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya kimaadili.
Julai
15-17 kitakuwa kipindi cha kukataa Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya
kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya Maadili ya TFF, Julai 18-22 itakuwa
siku ya kusikiliza rufaa za maadili na Julai 23 mpaka Julai 25 itakuwa
siku ya kutoa maamuzi ya Rufaa, Julai 26-28 kitakuwa kipindi cha kukata
rufaa dhidi ya kamati ya Uchaguzi kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya
TFF, rufaa hizo zitasikilizwa Julai 29 mpaka Agosti 2.
Wagombea
watajulishwa matokeo ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Agosti 5-6 itakuwa
siku ya kuchapisha majina ya wagombea watakaoingia kwenye Uchaguzi huo
na kampeni kwa wagombea zitaanza Agosti 7 mpaka 11 na siku inayofuata
yaani Agosti 12 itakuwa siku ya uchaguzi wa viongozi wa TFF.
Nafasi
zinazogombewa ni Rais wa TFF, Makamu wa Rais pamoja na nafasi 13 za
wajumbe TFF wanaowakilisha kanda 13 za Kagera na Geita; Mara na Mwanza;
Shinyanga na Simiyu; Arusha na Manyara; Kigoma na Tabora; Katavi na
Rukwa; Mbeya na Iringa; Njombe na Ruvuma; Lindi na Mtwara; Dodoma na
Singida; Pwani na Morogoro; Kilimanjaro na Tanga na Kanda maalum ya Dar
es Salaam.
Fomu za Urais zinapatikana kwa Sh. 500,000, Makamu wa Rais Sh. 300,000 na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji Sh. 200,000.
Next
This is the most recent post.
Previous
Ni miaka 10 imepita tangu Foe afariki dunia,Cameroon wanarudi Confedaration Cup.
Related Posts
Ni miaka 10 imepita tangu Foe afariki dunia,Cameroon wanarudi Confedaration Cup.
18 Jun 20170Ilikuwa ni mwaka 2003 nakumbuka pale nchini Ufaransa tukiishuhudia Cameroon ikiifunga Brazil na ...Read more »
Bifu kubwa laibuka kati ya Dani Alves na familia ya Maradona,sababu ni hii
18 Jun 20170Wiki iliyopita mlinzi wa kulia wa Brazil na klabu ya Juventus Dani Alves alikuwa akifanyiwa mahojia...Read more »
Unaonaje mpira ukibadilishwa na sheria hizi zikapitishwa?
18 Jun 20170The International Football Assosiation Board(TIFAB) ni asasi inayohusiana na masuala ya soka kim...Read more »
Movie kati ya Ronaldo na Manchester United yaanza upyaa
18 Jun 20170Hakuna ajuae hili movie litaisha lini kwani kila msimu wa usajili linaibuka, baada ya Ronaldo kus...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.