Wiki iliyopita mlinzi wa kulia wa Brazil na klabu ya Juventus Dani
Alves alikuwa akifanyiwa mahojiano na kitua kimoja cha habari nchini
Brazil, mahojiano ambayo yalidumu kwa muda wa lisaa lizima.
Wakati wa mahojiano hayo mwandishi wa habari alimuuliza swali Alves
ambalo limemuingiza matatani sana na familia ya nguli wa zamani wa soka
nchini Argentina Diego Maradona.
Muandishi alimuuliza Alves kuhusu ubora kati ya Lioneil Messi na
Diego Maradona ambapo Alves bila kupepesa macho alimtaja Lioneil Messi
na sio tu kumtaja bali akatoa sababu ya kutomkubali Maradona.
“Unaniuliza nani bora kati ya hao wawili?kwani Maradona amebeba tuzo
ya mchezaji bora wa dunia mara ngapi?Messi ni bora na huwezi jisifu wewe
ni bora wakati ulichukua kombe la dunia kwa goli la mkono” alisema
Alves.
Dani Alves alienda mbali zaidi kwa kumshambulia Maradona baada ya
kusema hawezi kuhadithia hata watoto wake jinsi alivyofunga goli la
mkono na huo sio mfano mzuri kwa wachezaji vijana.
Baada ya Alves kusema hivyo, mtoto wa kike wa Maradona aitwaye Dalma
Maradona hakutaka kuacha babake ashambuliwe vyote hivyo ikambidi achukue
simu yake na kujibu mashambulizi ya Alves.
“Hembu kaa chini na kawaulize Wabrazil wenzako watakuambia baba yangu
ni nani kwa jinsi alivyowanyanyasa na nina uhakika wao watakuambia
vizuri Maradona ni nani” alisema Dalma.
Dalma alisema kwanza swali la kumfananisha Maradona na Messi ni la
kipuuzi na kusisitiza baba yake alikuwa maarufu kipindi ambacho wanasoka
wemgi waliokuwa maarufu walikuwa wakitokea bara la Ulaya.
Dalma alizidi kumshambulia Alves kwa kumuambia kwamba baba yake
hakucheza soka ili kuwa Role Model wa mtu na kuhusu goli la mkono kama
hajalipenda baaasi aangalie magoli mengine.
Related Posts
NYAMLANI, MWAKALEBELA WAJITOKEZA KUJARIBU BAHATI URAIS TFF
18 Jun 20170Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ath...Read more »
Ni miaka 10 imepita tangu Foe afariki dunia,Cameroon wanarudi Confedaration Cup.
18 Jun 20170Ilikuwa ni mwaka 2003 nakumbuka pale nchini Ufaransa tukiishuhudia Cameroon ikiifunga Brazil na ...Read more »
Unaonaje mpira ukibadilishwa na sheria hizi zikapitishwa?
18 Jun 20170The International Football Assosiation Board(TIFAB) ni asasi inayohusiana na masuala ya soka kim...Read more »
Movie kati ya Ronaldo na Manchester United yaanza upyaa
18 Jun 20170Hakuna ajuae hili movie litaisha lini kwani kila msimu wa usajili linaibuka, baada ya Ronaldo kus...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.