The International
Football Assosiation Board(TIFAB) ni asasi inayohusiana na masuala ya
soka kimataifa, TIFAB imekaa na kuona kuna masuala ya sheria za soka
yanabidi kujadiliwa na kama ikiwezekana zibadilishwe.
Kubwa ambalo limekuwa gumzo ni suala la kupunguza muda wa kucheza
soka kutoka dakika 90 zinazotumika hivi sasa hadi kuwa dakika 60 ina
maana kila kipindi kitakuwa ni cha dakika thelathini thelathini.
TIFAB wana hoja kuhusu hili kwani wanadai wachezaji wanapoteza sana
muda wakiwa uwanjanj na hivyo ili kudhibiti suala hilo inabidi muda wa
kucheza uwanjani ubanwe na kupunguza kuwa dakika 60.
Idea nyingine ya TIFAB ni mchezaji kujipasia/kujianzia wakati akipiga
faulo au kona, sheria hii ni tofauti ya sasa ambapo ukianza mpira wa
free kick au kona ni lazima umpasie mchezaji mwingine ndio mpira
uendelee.
Sheria nyingine ya TIFAB wamependekeza kuwepo kwa saa ya uwanja
ambayo yenyewe itakuwa inaanza pamoja na ya muamuzi na kumaliza pamoja
na ile saa anayotumia muamuzi wa kati.
Pia TIFAB wametaka mpira wa free kick uwe unapigwa hata kama mpira
unatembea(sio lazima kusimama) na penati ikipigwa kama kipa akipangua
hairuhusiwi mchezaji mwingine kwenda kufunga.
Tayari sheria zilizopendekezwa na IFAB zimeanza kufanyiwa
majaribio,ikiwemo ya kapteni tu kuongea na muamuzi ambayo imeanza
kufanyiea majaribio katika michuano ya Confedaration Cup.
Related Posts
NYAMLANI, MWAKALEBELA WAJITOKEZA KUJARIBU BAHATI URAIS TFF
18 Jun 20170Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Ath...Read more »
Ni miaka 10 imepita tangu Foe afariki dunia,Cameroon wanarudi Confedaration Cup.
18 Jun 20170Ilikuwa ni mwaka 2003 nakumbuka pale nchini Ufaransa tukiishuhudia Cameroon ikiifunga Brazil na ...Read more »
Bifu kubwa laibuka kati ya Dani Alves na familia ya Maradona,sababu ni hii
18 Jun 20170Wiki iliyopita mlinzi wa kulia wa Brazil na klabu ya Juventus Dani Alves alikuwa akifanyiwa mahojia...Read more »
Movie kati ya Ronaldo na Manchester United yaanza upyaa
18 Jun 20170Hakuna ajuae hili movie litaisha lini kwani kila msimu wa usajili linaibuka, baada ya Ronaldo kus...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.