Meya
wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi
ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana
na madai ya kuwa na vyeti feki.
Jacob
pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya
utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.
Jacob
ameeleza kuwa kesi hiyo itasimamiwa na mawakili maarufu Tundu Lissu
ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Peter Kibatala..
Kesi hiyo itafunguliwa wiki ijayo baada mawakili hao kumaliza mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 18 mwaka huu ambapo Tundu Lissu ni mmoja wa wagombea wa kiti cha urais
Kesi hiyo itafunguliwa wiki ijayo baada mawakili hao kumaliza mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 18 mwaka huu ambapo Tundu Lissu ni mmoja wa wagombea wa kiti cha urais
Serikali yapiga marufuku kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa
katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua
kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia
kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia
kinyemela nchini.
Pamoja
na mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na
Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema
kuwa bila kuwa na takwimu sahihi za vizazi na vifo ama ndoa
inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.
“Wenzetu
nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi
bado tuko nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro kwa mujibu wa sensa ya
watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni
2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti vya kuzaliwa ni asilimia 11
pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” amesema.
Dk.
Mwakyembe pia ametumia nafasi hiyo kuwaonya watendaji wa mahakama
watakaolalamikiwa na wananchi kufanya kazi kinyume na maadili ikiwamo
upokeaji wa rushwa ama kutotenda haki na kutumia mahakama kugeuza kesi
za madai kuwa kesi za jinai.
Rais Magufuli atembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma na kufyatua matofali
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 16 Machi, 2017 ametembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino
Mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwaatahamia Dodoma hivi
karibuni kama alivyoahidi.
Mhe.
Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenister Joakim Mhagama na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi amesema pamoja na majengo ya Ikulu Serikali
itajenga miundombinu mingine zikiwemo reli na barabara za lami
zitakazounganisha maeneo ya vijiji vinavyozunguka Ikulu na mji wa
Serikali.
Pia
Mhe. Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa wote watakaoguswa na
shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Serikali na wanaostahili kulipwa
fidia watalipwa, na ametoa wito kwa wananchi hao kutumia fedha za fidia
watakazolipwa kujenga makazi bora na kujipanga kufanya shughuli zenye
manufaa kwao.
“Hapa
sasa watakuja watu wengi, wafanyakazi na wageni maana tayari Mabalozi
wa nchi mbalimbali nao watajenga ofisi zao hapa, sasa na nyinyi mjipange
kufanya biashara, mtapata soko la kuuza mazao na bidhaa nyingine,
mkipata fedha ziwasaidie kwa manufaa na sio kuzichezea” amesisitiza Mhe.
Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema
utekelezaji wa Serikali kuhamia Dodoma unakwenda vizuri ambapo mpaka
sasa viongozi wakuu wa wizara zote na wafanyakazi 2,069 wameshahamia
Dodoma na wengine wanaendelea kuhamia Dodoma.
Mhe.
Majaliwa ameongeza kuwa atasimamia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais
Magufuli aliyeagiza kujengwa kwa reli itakayounganisha eneo la Bwigili
na Dodoma mjini ili kurahisisha usafiri wa watu pamoja na kuharakisha
ujenzi wa barabara za kuzunguka mji wa Dodoma na barabara za kuunganisha
mji wa Serikali na Dodoma Mjini.
Wakiwa
katika eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa
wameshiriki ufyatuaji wa matofali yatakayotumia katika ujenzi wa majengo
ya Ikulu.
Mapema
kabla ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli amepokea taarifa ya
mapendekezo ya ujenzi wa Mji wa Serikali wa Makao Makuu Dodoma kutoka
kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mhandisi
Paskasi Muragili na kuagiza ujenzi wa Mji huo uzingatie maslai ya Taifa.
Post a Comment