Akufukuzaye, hakuambii toka. Lakini kwa
Kocha, Arsene Wenger inaonekana imezidi kupita kiasi. Maana sasa
mashabiki wa Arsenal wameamua kutembeza matangazo mtaani.
Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekodi gari la matangazo lenye ujumbe unaoonyesha umefika wakati wa Wenger kuwaachia timu yao.
Mashabiki hao wanasisitiza Wenger aachie ngazi kwa kuwa wamechoka katokana na mwenendo wake.
Kama hiyo haitoshi, mashabiki hao
wanaendelea kusisitiza wamekuwa wakisubiri mafanikio ya kubeba angalau
ubingwa barani Ulaya, sasa ni mwaka wa 20 lakini hakuna mafanikio.
Hasira za mashabiki hao zimeamka zaidi
baada ya Wenger kuonekana anataka kuongeza muda na yuko katika hatua za
mwisho kusaini tena mkataba.
Post a Comment