Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF anayetambulika na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa nchini Prof. Ibrahim Lipumba
amesema ameandika barua maalumu kwa jukwaa la wahariri kuonesha
kusikitishwa kwake na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika mkutano wa CUF na kusababisha waandishi kufanyiwa fujo.
Prof Lipumba ameliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ameyasema hayo katika mahojiano na mwandishi wa habari wa Azam Two na pamoja na mambo mengine amemtaka katibu mkuu wa CUF Maalim Seif wakae wazungumze ili wamalize tofauti zao na wakae wakijenge chama..
“Baada ya kulisikia hilo
niliamua kuchukua jukumu la kuwaandikia Jukwaa la wahariri barua ambayo
ipo mbioni kwenda kwenye ofisi zao kwamba mimi binafsi kama mwenyekiti
wa CUF nalaani kitendo cha kupigwa kwa waandishi wa habari na nijambo
ambalo hatulikubali kabisa, hatuwezi kujenga Demokrasia ikiwa waandishi
wahabari hawafanyi kazi yao katika hali ya amani na utulivu”
“Vile vile kijana wetu amekatwa
kisigino kwa panga na anavyo elewa yeye kijana aliyemkata anaitwa
Mohamedi Mgonvi na taarifa hii imepelekwa kwenye vyombo vya dola kwaiyo
vyombo vya dola inalishughulikia na tulitoa wito ambao ulitolewa na
Mkurugenzi wetu wahabari na uwenezi”
“Mimi toka awali nimeeleza
kwamba nataka tumalize tofauti za kisiasa kwa mazungumzo tupate suluhu
tuheshimu katika ya chama chetu na nimekuwa nikimuita Maalim Seif aje
ofisi bugurudi aweze kuzungumza afanye kazi zake kama katibu mkuu na
mimi nimemfahamu Maalim Seif mwaka 1973 tukiwa wanafunzi wa chuo kikuu
Dar es Salaam kwahiyo hatuna sababu ya sisi kuwa na mgogoro huu na
kuuruhusu kuendelea”
“Hivi sasa kupitia taarifa zetu
zakiuchunguzi zinaonesha kwamba kuna mbinu yakutaka chama hiki kiweze
kufutwa kwaiyo kuna matukio ya napangwa njee ya chama ili paweze kutokea
vurugu nazikishatokea waseme chama hiki hakifai kuendelea kuwa chama
cha siasa na utakuta kuna vyama vingine vya siasa vinashabikia na kutoa
wito ilichama hichi kiweze kufutwa” Prof. Lipumba
Home
»
»Unlabelled
» Siasa “kuna mbinu yakutaka chama hiki kiweze kufutwa” Prof Lipumba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment