Rapa kutoka Marekani Nicki Minaj ametangaza kupitia twitter yake kuwa kama kuna mwanafunzi anahitaji msaada, aonyeshe ushahidi wa kufaulu kwa alama ‘A‘ na ataweza kupata msaada.
Kauli hii imetoka kwa Nicki baada ya kuombwa msaada na mwanafunzi mmoja nchini Marekani aliyetaka kusaidiwa kulipa ada ya chuo na Minaj.
Nicki ameandika “Show me straight A’s that I can verify w/ur school and I’ll pay it. Who wants to join THAT contest?!?! Dead serious. Shld I set it up?
Wanafunzi wanaohitaji misaada tofauti walianza kumtumia Minaj matokeo yao na inasemekana kuwa tayari pesa zaidi ya dola 1000 zimetumwa kwa wanafunzi wawili waliotaka pesa za vitabu

Post a Comment

 
Top