Hatma
ya Malimi Busungu kubaki Yanga inasubiri majaliwa ya Kocha George
Lwandamina ambaye ameomba CD za mechi zote za timu hiyo ili kuangalia
kiwango cha kila mchezaji kisha aamue kama atambakisha ama la.
Busungu
alishakubali kuondoka Yanga katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha
dogo na baadhi ya timu zilipanga kumsajili kwa mkopo baada ya kuona hana
nafasi katika kikosi cha kwanza.
Hata
hivyo, Lwandamina, raia wa Zambia, aliyejiunga na Yanga akitokea Zesco
ya nchini kwao, ameagiza kutofanyika jambo lolote la usajili kwa sasa
hadi atakapoona viwango vya wachezaji wake.
Meneja
wa Busungu, Yahya Tostao, alisema awali kulikuwa na mchakato wa kumtoa
kwa mkopo Busungu na timu nne zilionyesha nia ya kumhitaji.
“Mambo
yote yamesimama kwanza kwani Lwandamina anataka kwanza kupitia CD za
mechi zote ili kufahamu kama atamhitaji (Busungu) kwa ajili ya kufanya
naye kazi ama la.
“Iwapo
hatamhitaji, itabidi tuendelee na mpango wa kumpeleka kwa mkopo katika
timu nyingine, kwa sasa bado tunaendelea na mazungumzo na timu
zinazomhitaji Busungu,” alisema Tostao.
Post a Comment