Kocha Hans van der Pluijm, amesema suala la nani bosi haliwezi kuwa kitu muhimu, badala yake ushirikiano wake yeye na George Lwandamina ndiyo jambo bora zaidi.
Pluijm amepanda cheo na kuwa mkurugenzi wa ufundi wa Yanga, wakati Lwandamina anachukua nafasi yake kama kocha mkuu.
"Lengo ni mafanikio ambayo yatazaliwa na ushrikiano, nani bosi nani mkubwa haliwezi kuwa suala la msingi sana. Mwisho wa msimu, tunatakiwa kuwa na mafanikio," alisema.
Jana,
rasmi Yanga ilimtambulisha Lwandamina kuwa kocha wake mkuu pia
ikamtambulisha Pluijm kuwa mkurugenzi wa ufundi, klabu hiyo imesema
Pluijm ni bosi wa Lwandamina.
Awali
kulikuwa na sintofahamu kuhusu nafasi ya Pluijm raia wa Uholanzi kwamba
labda angekuwa chini ya Lwandamina raia wa Zambia aliyejiunga na Yanga
akitokea Zesco ya nchini kwao.
Akimtambulisha
kwa waandishi wa habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga,
alisema Lwandamina ni kocha mkuu atakayekuwa chini ya Pluijm ambaye yeye
atakuwa akizitazama timu zote za Yanga.
“Pluijm
yeye ni bosi wa timu zote za Yanga kuanzia hii ya wakubwa hadi ile ya
vijana na nyingine zitakazoanzishwa, ila majukumu ya Pluijm kwa
Lwandamina yataishia nje ya uwanja.
“Ndani
ya uwanja kwa timu ya wakubwa bosi atakuwa Lwandamina na hataingiliwa
na Pluijm labda kushauriwa tu, hivyo ndivyo watakavyofanya kazi,”
alisema Sanga.
Akizungumza
baada ya kutambulishwa, Pluijm alisema atahakikisha anafanya kazi bega
kwa bega na Lwandamina ili kuipa mafanikio Yanga kuanzia pale alipoachia
yeye.
“Nitafanya
naye kazi kwa karibu kwa manufaa ya Yanga na Tanzania, naamini tutakuwa
na matokeo mazuri ya pamoja hivyo mashabiki wasiwe na wasiwasi,”
alisema Pluijm.
Kwa
upande wake, Lwandamina alisema: “Nitajitahidi kufanya kazi pamoja na
Pluijm kuhakikisha Yanga inapiga hatua zaidi kutoka mahali ilipo sasa.”
Post a Comment