![]() |
MOHAMMED DEWJI |
Ile
ishu ya bilionea shabiki wa Simba, Mohammed Dewji kumwaga mamilioni ya
fedha kusaidia usajili wa kuwabakiza wachezaji Ibrahim Ajibu, Jonas
Mkude na Mohamed Zimbwe, umeonekana kuwa faraja kwa mashabiki wengi wa
Simba.
Badaa
ya kuripotiwa jana, mashabiki wengi wamekuwa wakianzisha mjadala
mitandaoni kwamba, wana imani wachezaji hao watabaki Msimbazi.
Tayari Simba imefanikiwa kumsainisha Zimbwe Jr maarufu kama Tshabalala mkataba wa miaka miwili.
Lakini mashabiki wengi walikuwa na hofu ya kuwakosa Ajibu na Mkude ambao tayari walionyesha wako tayari kwenda hata Yanga.
Hata hivyo kumekuwa na taarifa kuwa Ajibu, amekataa kusaini hadi mkataba wake utakapoisha ili aende akacheze nje ya Tanzania.
Lakini
katika mijadala hiyo ya mitandaoni, wengi wanasema Ajibu alikuwa
‘anatikisa kiberiti’ kwa kuwa anataka kupata fungu la kutosha.
Taarifa
nyingine zimeeleza, kamati ya usajili ya Simba, tayari imeanza
mazungumzo na Ajibu na Mkude ili kufikia mwafaka ili waongeze mkataba
kabla ya mwisho wa msimu na ikiwezekana kabla ya kuanza kwa mzunguko wa
pili.
Post a Comment