GIDABUDAY (KULIA) |
Chama cha Riadha
Tanzania (RT), jana Jumapili kilifanya uchaguzi wake mkuu na kuwapata
viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho kwa miaka minne ijayo.
Katika uchaguzi huo
uliofanyika kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar, Anthony Mtaka
alichaguliwa kuwa rais, William Kalaghe (Makamu wa Rais - Utawala), Dk
Ahmed Ndee (Makamu wa Rais - Ufundi), Wilhelm Gidabuday (Katibu Mkuu),
Ombeni Zavala (Katibu Mkuu Msaidizi) na Gabriel Liginyani (Mweka
Hazina).
Waliochaguliwa kuwa
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lwiza Msyani, Meta Bare, Rehema Killo,
Dk Nassor Matuzya, Robert Kalyahe, Zakaria Buru, Mwinga Sote, Tullo
Chambo, Christian Matumbo na Yohana Mesese.
Akizungumza baada
ya uchaguzi huo, Mtaka alisema atahakikisha anaanza kazi mara moja
kuhakikisha mchezo wa riadha unapiga hatua kubwa kutoka hapo ulipo
kufika anga za juu zaidi.
“Nitahakikisha nashirikiana na wajumbe wenzangu kuufanya mchezo huu kufika levo za juu,” alisema Mtaka.
Post a Comment