WASANII maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Nassib Abdul ‘Diamond’ na Ali ‘King’ Kiba watarekodi pamoja wimbo maalum wa kuhamasisha kampeni za kuchangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys.
Hayo
yamesemwa leo na Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge
wakati wa mkutano na Waandishi wa Habari leo mchana Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam kuzungumzia mikakati yao ya kukusanya fedha kwa ajili ya
kuisaidia timu hiyo.
Kitenge amesema kwamba tayari ala za wimbo huo zimekwishatengenezwa na wasanii hao wote wametumiwa kwa ajili ya kuingiza sauti, ili mara moja wimbo huo ukamilishwe na kuanza rasmi kusaidia kampeni ya kuhamasisha Serengeti Boys.
Mjumbe wa Kamati ya Serengeti Boys, Maulid Kitenge akizungumza leo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
“Ali Kiba yuko Marekani na tayari amekwishatumiwa ala za wimbo ili aingize sauti. Na Diamond yeye yupo hapa nchini na tayari ametumiwa ala hizo ili aingize sauti. Wote wameahidi kufanya hivyo mara moja na kurejesha kazi hizo, ili na wasanii wengine waingize sauti zao,”amesema.
Kitenge amewataja baadhi ya wasanii wengine ambao wataingiza sauti zao kwenye wimbo huo kuwa ni Mwasiti Almasi, Darasa na Vanesa Mdee.
Kiba na Diamond wote wapo kwenye Kamati iliyoundwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ya kuhamasisha na kuwaunganisha Watanzania kwa pamoja ili kuichangia Serengeti Boys iliyofuzu Fainali za Afrika nchini Gabon Mei mwaka huu.
Katibu wa Kamati hiyo ni Mwesigwa Selestine ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakati wajumbe ni Kitenge wa EFM Radio na TV, Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Mrembo wa Tanzania wa mwaka 1999, Hoyce Temu.
Pia wamo Mkurugenzi wa Habari katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hassan Abbas; Mkurugenzi wa Global Publishers Limited, Eric Shigongo na Mkurugenzi wa Radio Clouds, Ruge Mutahaba.
Pamoja na hayo, katika kongamano hilo na wadau wa soka wadau ikiwamo Serikali iliridhia kuwa mshiriki wa karibu kwa kila hatua kuanzia Bodi ya Mfuko wa Maendeleo ya timu za taifa, Kamati ya Hamasa kwa lengo la kupanga pamoja na kushirikiana kwa pamoja.

ZANZIBAR SASA MWANACHAMA KAMILI CAF
CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimepata uanachama kamili wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa mujibu wa habari kutoka Addis Ababa, Ethiopia.
Kwa maana hiyo, Zanzibar inatengana moja kwa moja moja Tanzania Bara katika mashindano yote ya CAF.
Mkutano Mkuu wa 39 wa CAF unaoendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia tangu jana umeafiki kuipa Zanzibar uanachama kamili baada ya awali kuipa uanachama wa muda kama mwanachama mshiriki.
ZFA ilianzishwa mwaka mwaka 1949 na kipindi chote mbali ya kuwa sehemu ya Tanzania kisoka, imekuwa ikishiriki michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) tu kama nchi.
Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limempongeza Rais mpya wa CAF, Ahmad Ahmad baada ya kumshinda rais wa muda mrefu, Issa Hayatou kwa kura 34 kwa 20.

WATANZANIA WAOMBWA KUICHANGIA SERENGETI BOYS KUPITIA NAMBA HII MITANDAO YOTE
WATANZANIA
wameombwa kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17,
Serengeti Boys kupitia namba 223344 kwa ajili ya maandalizi yake ya
kushiriki Fainali za Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel, Beatrice Singano ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kusaidia Serengeti Boys katika Mkutano na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
“Kwa kila mwenye moyo wa kuchangia anaweza kuchangia kupitia namba 223344 na namba hii itatumika katika mitandao mitatu ambayo ni Airtel, Tigo pamoja na Vodacom. Na jinsi ya kulipia utalipia kwa njia ya Selcom malipo kupitia mtandao husika, kupitia mtandao wa Airtel unapiga *150*60# na tigo *150*01# na Vodacom *150*01#”alisema Beatrice.
Beatrice Singano akizungumza na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo
Mwenyekiti wa Kamati ya Serengeti Boys, Charles Hillary akizungumza leo
Amesema pia kutokana na umahiri Serengeti Boys waliouonyesha katika michezo ya awali ana uhakika timu hiyo itafanya vizuri katika fainali hizo, hivyo kuwataka Watanzania kuwa bega kwa bega na kikosi hicho.
Mapema kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Charles Hillary alisema kwamba wameorodhesha makampuni mbalimbali waliyoyaomba kuichangia Serengeti Boys.
Hillary amesema kwamba watabisha hodi pia na Halmashauri za Wilaya zote nchini kwa msaada wa Serikali na huko wanatarajia kupata Sh.Milioni 100.
Na akasema si wote watakiwa kuchangia fedha, bali wengine watatoa misaada mingine inayohitajika wakati wa maandalizi ya timu kwenda Fainali za Gabon, ikiwemo tiketi za ndege, kambi, vyakula na kadhalika.
Serengeti Boys ipo kambini kwa wiki mbili sasa katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kikiendelea na maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki itakayo chezwa mkoani Kagera kabla ya kwenda mjini Rabat, Morocco kwa kambi ya mwezi mmoja ikiwa ni maandalizi ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazo fanyika nchini Gabon Mei 14 mwaka huu.

Post a Comment