Msanii wa bongofreva kutoka Dodoma James Mgala a.k.a Jimmy Yeyoo  anayetamba na kibao cha Ringa alichomshirikisha mwanadada kutoka Uganda Agycox amesema hapendi kitendo cha baadhi ya wasanii wanaojisikia/wanaolinga,,

 Jimmy amesema hayo alipokuwa anahojiwa na Mtangazaji wa Redio Jamii fm Morogoro.Andrew Mbwiga kupitia kipindi cha Combination Dj 1416  Amesema wasanii wadogo wanapitia changamoto kubwa sana pale wanapohitaji kufikia malengo yao kuanzia kurekodi,collabo na promotion ya Nyimbo zao
Lakini pia amesema kutokana na Mziki kubadilika kuwa wa biashara kunapelekea mziki kukosa ubora na kukosa wasanii wenye vipaji
Hata hivyo amewaomba maproduza kufanya kazi na watu wenye vipaji na siyo kuangalia hela pekee...Jimmy yeyoo alianzia Mziki Mkoani Bukoba kutokana na Maisha ya  shule alihamia Dodoma na kuendeleza na Elimu ya Chuo kikuu (UDOM) baada ya kuhitimu na kuajiliwa Dodoma kama Mwalimu wa sekondari akaendelea na harakati za Mziki.

Post a Comment

  1. True brother, na sio wasanii tu hata maredio presenters wanafanya wasanii wadogo waisome namba wakitafta kutoboa.

    ReplyDelete

 
Top