Mashuhuda  wa ajali iliyosababisha kifo cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya wamesema alikufa kutokana na kushindwa kupewa msaada kwa haraka.

Walisema baada ya ajali walisikia sauti za watu wakilia kuomba msaada lakini ilichukua muda wa sasa tatu ndipo walipopata msaada wa kuokolewa kutokana na ukosefu wa vifaa vya uokoaji.

Juzi katika eneo la Emmaus mkoani hapa ilitokea ajali ya gari la Toyota Noah na lori ambayo ilichukua maisha ya Mwenyekiti huyo na watu wengine watatu kujeruhiwa. 
Mmoja wa mashuhuda hao Amri Juma alisema alisikia sauti za wanawake wakiomba msaada ili waweze kuokolewa.

“Ni jambo la kusikitisha kuona zaidi ya saa tatu hakuna vifaa vya uokoaji vilivyokuwa vimefika kwa ajili ya uokoaji, ajali ilitokea saa nane mchana lakini mpaka saa 11 jioni ndio watu wanakuja kutolewa.

‘’‘Breakdown moja ilipofika ilishindwa kunyanyua lori, ilipofika ya pili ilishindwa, hali inayoonesha kuna uhaba wa vifaa hivyo mamlaka husika zijipange kuw

Post a Comment

 
Top