![]() |
Didier Drogba |
Kocha huyo Mauro Biello anayeifundisha Montreal amethibitisha staa huyo kutoridhia kucheza mchezo dhidi ya Toronto akitokea benchi.
"Niliongea nae Jumamosi lakini alionekana kutoridhia suala la kutokea benchi na kucheza kwa dakika 18 za mwisho hivyo akaona bora kutocheza kabisa"
Drogba alitaka kuanzishiwa benchi kutokana na kurejea akitokea majeruhi hivyo kocha hakutaka aanze kikosi ch kwanza moja kwa moja kitu ambacho hakikumpendeza Drogba
Staa huyo alijiunga na Montreal 2015 akitokea Chelsea na amefanikiwa kuichezea Mechi 35 na kufunga Magoli 21
katika mechi nne za mwisho za Montreal Drogba ametolewa katika mechi mbili,klabu ya montreal inayoshiriki ligi kuu marekani MEJOR LEAGUE Ililazimishwa sare ya kufungana goli 2-2 na Toronto Drogba kwa sasa ana umri wa miaka 38 na yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha soka lake la kulipwa.
Post a Comment