NAHODHA wa zamani wa England, David
Robert Joseph Beckham leo ametua Tanzania akiwa na familia yake, mkewe,
Victoria Adams ‘Posh’ na wanawe, Brooklyn Joseph, Romeo James, Cruz David na
Harper Seven.
Beckham, kiungo wa zamani wa Manchester United, Preston North End, Real Madrid, AC Milan, LA Galaxy na Paris Saint-Germain ameonekana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwasili na familia yake leo.
Hata hivyo, Bekcham hakutaka kuzungumza chochote juu ya ujio wake na alipotoka nje alipokewa na wenyeji wake, moja kwa moja kuelekea kwenye gari na kutokomea kusikojulikana, ingawa ni katikati ya mji.

MKUDE APATA AJALI MBAYA DUMILA, LAKINI YUKO SALAMA
NAHODHA wa Simba, Jonas Mkude amenusurika katika ajali mbaya ya gari iliyotokea eneo la Dumila mkoani Morogoro mchana wa leo.
Mkude na watu wengine watano akiwemo dereva walikuwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 wakisafiri kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam.
Na walipofika Dumila tairi la mbele likapasuka na gari hiyo kupoteza mwelekeo hadi kwenye pori upande wa kushoto.
Abiria mmoja aliyatajwa kwa jina la Shose Fiderine ndiye aliyeumia zaidi, lakini hata Jasmin, Mkude na dereva ambaye pia ndiye mmiliki wa gari ajulikanaye kwa jina la utani, Rais wa Kibamba nao wameumia.
Wanachama wa Simba waliokuwa kwenye basi dogo wakirejea Dar es Salaam walipofika eneo la tukio walisimama kutoa msaada. Mkude alikuwa anatoka Dodoma, ambako jana aliisaidia Simba kukata tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Katika fainali kali na ya kusisimua ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), dakika 90 zilimalizika timu hizo zikiwa hazijafungana na mabao matatu yakapatikana katika dakika 30 za nyongeza, Simba mawili, Mbao moja.
Wachezaji Frederick Blagnon raia wa Ivory Coast na Robert Ndaki ambao wote walitokea benchi kipindi cha pili ndiyo waliokwenda kuzifungia mfululizo timu zao.
Blagnon alianza kuwainua vitini mashabiki wa Simba dakika ya 95 baada ya kumzidi maarifa beki wa Mbao FC kufuatia pasi ndefu ya beki wa kushoto pia, Abdi Banda.
Lakini Ndaki akaisawazishia Mbao dakika ya 109 akitumia makosa ya Banda aliyezubaa akidhani mfungaji kaotea.
Wakati wengi wanaamini mchezo utaamuliwa kwa mikwaju ya penalti, lakini refa Ahmed Kikumbo akawazawadia Simba penalti baada ya beki mmoja wa Mbao FC kuunawa mpira uliopigwa na Abdi Banda dakika 119.
Wachezaji wa Mbao FC walimzonga refa huyo kabla ya kuamua kutulia na kukubali mchezo uendelee, ndipo winga Shiza Ramadhan Kichuya akaenda kuifungia Simba bao la ushindi na kuamsha shangwe na nderemo Uwanja wa Jamhuri, Dodoma. Wakati kikosi cha Simba kimebaki Dodoma kwa ajili ya kwenda kuonyesha Kombe lao Bungeni kesho na baadaye kwenda kucheza mechi ya kirafiki Singida, Mkude na wachezaji wengine wa Simba walioitwa timu ya taifa wamelazimika kuondoka leo kwa usafiri tofauti kurejea Dar es Salaam kujiunga na Taifa Stars.
Mkude aliomba lifti kwa rafiki yake, Rais wa Kibamba wakati wengine akiwemo beki Abdi Banda walipanda mabasi. Wengine walioitwa Taifa Stars kutoka Simba ni beki Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, viungo Said Ndemla, Kichuya, Muzamil Yassin, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim na mshambuliaji Ibrahim Hajib.
NDIKUMANA YUKO TAYARI KUUNGANA NA MAVUGO SIMBA SC
KIUNGO wa ulinzi wa kimataifa wa Burundi, Youssouf Ndikumana amesema kwamba yuko tayari kujiunga na washindi wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba SC iwapo watafika bei yake.
mchezaji huyo wa Mbao FC ya Mwanza alisema kwamba kwake anaangalia maslahi na kama Simba wataweza kutoa kiwango cha fedha anachotaka atajiunga nao. "Mimi nipo tayari kujiunga Simba au timu yoyote kati ya hizo zinazotajwa zinanitaka, kikubwa ninaangalia maslahi," alisema.
Ndikumana alicheza vizuri jana katika fainali ya ASFC, ingawa Mbao FC ililala 2-1 mbele ya Simba SC Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Na wakati tayari kuna tetesi za mchezaji huyo kutakiwa na Simba SC, naye amesema yuko tayari kwenda kuungana na Mrundi mwenzake, mshambuliaji Laudit Mavugo.
Singida Utd mbioni kuibomoa Simba, yamnyakua Ajib, wawili zaidi kufuata
klabu ya Singida United iliyopanda daraja imezidi kuonesha dhamira ya kufanya vizuri msimu ujao kwa kuendelea kufanya usajili wa nguvu.Baada ya kuwatikisa mabingwa wa Ligi za Kenya na Zimbabwe, Tusker n CAP United, mara hii wamewatikisa mabingwa wa Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, Simba kwa kumalizana na mshambuliaji wao Ibrahim Ajib.
Pande mbili zimemalizana na kukubaliana kila kitu na sasa wanasubiri tu kumtambulisha rasmi Ajib kwa umma.
Hata hivyo Simba inaonekana kutoshtushwa na kuondoka kwa Ajibu kwani ni kama tayari imejipanga kwa kumalizana na John Bocco ambaye takwimu zinaonesha ni mfungaji bora zaidi ya Ajib.
Kama vile haitoshi, Singida United wako katika mazungumzo ya kumchukua kiungo muhimu wa Simba anayemaliza mkataba wake pamoja na kipa Peter Manyika.
Fainali ya Simba na Mbao yaweka rekodi ya mapato
Pambano la fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, kati ya Mbao na wekundu wa Msimbazi, Simba lililopigwa Jumamosi katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma limevunja rekodi ya mapato baada ya kuingiza shilingi milioni 117. Kiasi hicho kimetokana na watazamaji takriban 15,000 waliokuwa na kiu ya pambano hilo la fainali lililomalizika kwa ushindi wa Simba wa mabao 2-1 uliopatikana kwenye muda wa ziada.Rekodi ya mapato katika uwanja huo uluofanyiwa marekebisho katika dimba la kuchezea ilikuwa ni shilingi milioni 68.
Ukiondoa mechi za watani wa jadi, kiasi hicho ni kikubwa kuliko mapato ya mechi nyingine za Ligi na Kombe la Shirikisho zilizochezwa msimu huu.
Msimu huu mapato yameshuka kwa asilimia kubwa kiasi cha mechi kubwa kama Yanga na Mtibwa kushindwa kuingiza zaidi ya milioni 10 jijini Dar.
Baada ya mapato ya mechi za Dar kuporomoka sana , michezo ya mikoani inayohusisha Simba na Yanga ndio inaongoza kwa mapato makubwa huku rekodi ikishikiliwa na pambano baina ya Mbeya City na Simba lililoingiza kiasi cha shilingi milioni 60 Oktoba mwaka jana.
Umemsikia Shiza Kichuya?
Winga teleza wa Simba SC Shiza Ramadhani Kichuya ameisifu klabu yake na kujisifu kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo.Kichuya anasema licha ya kulikosa kombe la ligi lakini ana mshukuru Mungu wao kunyakua kombe la ASFC na kuiwezesha timu yao kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika kombe la Shirikisho mwakani.
” ni miaka mingi klabu ilikuwa haijafuzu kwa michuano ya CAF kwahiyo kuwepo katika kikosi ambacho kimeirudisha timu katika michuano hiyo ni jambo la kumshukuru Mungu na sisi sote wachezaji na viongozi limetupa faraja kubwa ”
Shiza Kichuya amejiunga na Simba SC msimu huu akitokea Mtibwa Sugar na amefanikiwa kupata namba ya kudumu katika kikosi hicho kama winga wa kileo.
Goli lake la jana kunako dakika ya 112 muda wa nyongeza dhidi ya Mbao akimtungua kipa wa Mbao Mirunda kwa mkwaju wa penati , ndio goli la ushindi lililowafanya Simba kumaliza mchezo kwa matokeo ya 2-1 . Goli la kwanza la Simba SC lilifungwa na Blagnon.
SAMATTA AFIKISHA MABAO 20 GENK IKIUA 3-0 UBELGIJI
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana amefunga bao la tatu timu yake, KRC Genk ikishinda 3-0 ugenini dhidi ya Sint-Truiden Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Ubelgiji kwenye mchezo wa Kundi B kuwania tiketi ya kucheza michuano ya UEFA Europa League mwakani.
Hilo linakuwa bao lake la 20 Samatta katika mechi 59 tangu ajiunge na Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya DRC. Na kwa ushindi huo, Genk inaendelea kuongoza Kundi B katika kuwania tiketi ya Europa League 2018 ikifikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 10.
Samatta alifunga lake dakika ya 55 jana akimalizia pasi ya beki wa Jamhuri ya Czech, Jakub Brabec, baada ya kiungo mkongwe Mbelgiji mwenye umri wa miaka 36 Thomas Buffel kufunga la kwanza dakika ya 32 na kiungo Mholanzi, Jean-Paul Boetius kufunga la pili dakika ya 43. Kati ya mechi hizo 59, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 41 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 37 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 27 msimu huu.
Mechi 21 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 13 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, tano msimu uliopita na sita msimu huu na katika mabao hayo 19, 14 amefunga msimu huu na tano msimu uliopita.

Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.